Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: YANGA SC WAKIMATAIFA WARUDI KILELENI BAADA YA KUITANDIKA MTIBWA 1 - 0 UWANJA WA TAIFA
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Anza na hii, timu ya Arsenal mara nyingi inashindwa kufika kileleni karibuni miaka 12 sasa kila wa...
Anza na hii, timu ya Arsenal mara nyingi inashindwa kufika kileleni karibuni miaka 12 sasa kila wakijitahidi wanashindwa kufika kileneni tatizo la Arsenal linafahamika huwezi kufika kileleni kama washambuliaji wako butu leo Yanga imerudi kileleni mwa ligi kuu kwa kufika alama 59 nyuma ya Simba yenye alama 57
Saimon Msuva
YANGA NA MTIBWAKwa hakika wote wamecheza mpira mzuri ushindi wa Yanga haukuwa rahisi kama ulivyo tarajiwa kwani walijitahidi kuzuia mashambulizi ya Mtibwa wakati wote, Huenda Malim Busungu angekuwa makini Yanga wange andika mabao zaidi kwani nafasi amezipata ameshindwa kuzitumia Daki ya 47 Saimon Msuva amehakikisha Yanga inapata alama tatu muhimu na kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi.

Michezo iliyo baki michache kila mmoja ana uwezo wa kuwa bingwa wa ligi hiyo, ligi ilipo fikia patamu sana ukiangalia kwa jicho dhaifu unaweza kusema timu moja inachukua ubingwa ila ligi bado mbichi mno yoyote anaweza kuibuka bingwa.

Michezo MingimeCoastal Union Waarabu wa Tanga wamepata alama Tatu muhimi leo kwa kuifunga Jkt Ruvu goli 1-0 wakati Kagera Sugar wamelala kwa Ndanda fc kwa magoli 2-0.

MATOKEO KWA UJUMLA KWA MECHI ZILIZOPIGWA LEO
Yanga 1 - 0 Mtibwa
Ndanda 2 - 0 Kagera Sugar
Coastal Union 1 - 0 Jkt Ruvu

MSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA
NamePWDLGFGAGDPts
Young Africans24185157134459
Simba SC24183343133057
Azam FC24167141162555
Mtibwa Sugar26127729191043
Tanzania Prisons26101152321241
Mwadui FC2697102525034
Stand United25104112222034
Ndanda FC2771282627-133
Majimaji2696112034-1433
Mbeya City2686122833-530
Toto Africans2669112436-1227
Kagera Sugar2767141831-1325
JKT Ruvu2566132438-1424
Mgambo JKT2658132032-1223
African Sports2765161130-1923
Coastal Union2757151536-2122

About Author

Advertisement

 
Top