Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: WAZIRI MKUU AOMBWA NA CUF KUINGILIA MGOGORO WA UMEYA JIJI LA TANGA
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Chama cha wananchi CUF kimemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuingilia mgogoro wa umeya katika ji...
Chama cha wananchi CUF kimemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuingilia mgogoro wa umeya katika jiji la Tanga baada ya juhudi mbalimbali za kudai haki kugonga mwamba.
Chama cha wananchi CUF
Akizungumza jijini Dar es Salaam Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF bara Magdalena Sakaya ameeleza kuwa ni vyema waziri mkuu akatumia busara kama alizotumia Rais Magufuli kumaliza mgogoro wa umeya katika jiji la Dar es Salaam, ili kuanza kwa vikao vya Baraza la Madiwani wa jiji la Tanga ambalo limesusiwa.

Katika hatua nyingine Sakaya amesema kuwa jeshi la polisi limekuwa likitumia nguvu ya dola kuzuia shughuli zote za kisiasa za CUF ikiwemo mikutano ya nje na ya ndani, huku ya Chama cha Mapinduzi CCM ikiruhusiwa, jambo ambalo linakidhoofisha chama hicho na madiwani wake.

Mgogoro huo wa umeya umetokea kufuatiwa kile kinachodaiwa kuchakachuliwa kwa matokeo ya CUF na kupewa ushindi kwa chama CCM cha katika uchaguzi uliofanyika Desemba 19 2015 ambapo CUF wakiwakilishwa na Rashid Jumbe walipata kura 20 huku CCM wakiwakilishwa na Selemani Mustafa walipata kura 17.

Sakaya amezidi kueleza kuwa matokeo hayo yalipinduliwa na mkurugenzi wa jiji la Tanga ambaye kwasasa amehamishwa Daudi Mayeji na kusomeka kuwa CCM 19, CUF 18, ambapo wakala wa CUF Khalid Rashid alipinga palepale kwani alidai matokeo yalikuwa CCM 17 CUF 20 baada ya zoezi la kuhesabu kura kurudiwa.

Unaweza kumsikiliza Hapo chini Magdalena Sakaya Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara kuhusiana na Sakata la Umeya Tanga

About Author

Advertisement

 
Top