Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: WATU ZAIDI YA 28 WAUAWA KABUL KATIKA TUKIO LA KIGAIDI
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Watu zaidi ya 28 wameuawa na wengine zaidi ya 300 kujeruhiwa baada ya kutokea mlipuko wa bomu Juman...
Watu zaidi ya 28 wameuawa na wengine zaidi ya 300 kujeruhiwa baada ya kutokea mlipuko wa bomu Jumanne hii kwenye mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani wa nchi hiyo, Sediq Sediqi amesema mtu aliyejitolea mhanga alijilipua akiwa kwenye gari.

Afghanistan
Shambulio hilo liliilenga ofisi ya timu ya ulinzi inayowalinza viongozi wakubwa wa serikali. Ofisi hiyo ipo chini ya ofisi ya rais ya masuala ya utawala. Kundi la Taliban limekiri kuhusika kwenye tukio hilo.
Kabul
Rais Mohammad Ashraf Ghani amelaani kutokea kwa shambulio hilo.
“Today’s terrorist attack near Pul-e-Mahmud Khan, #Kabul clearly shows the enemy’s defeat in face-to-face battle with (Afghan National Defence and Security Forces),” alitweet Ghani.

About Author

Advertisement

 
Top