Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA MKOANI LINDI, MMOJA AKIJINYONGA NA MWINGINE KUSOMBWA NA MAJI MTO MBWEMKURU
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Mnamo tatehe 19.4.2016 majira ya saa moja na nusu jioni mtaa wa mitandi uliyopo Manispaa ya Lind...
Mto Mbwemkuru
Mnamo tatehe 19.4.2016 majira ya saa moja na nusu jioni mtaa wa mitandi uliyopo Manispaa ya Lindi  ndg Amina Abdala mwenye miaka 30, mwenye asili ya kabila ya kimakonde aligundua kujinyonga kwa mme wake aliyetambulika kwa jina moja la Khatibu mwenye miaka 30, ambaye kabila lake ni mmwera.

Mtu huyo alijinyonga kwa kutumia kamba aina ya manila nje ya nyumba yake na sababu za kujinyonga bado hazijafahamika, mwili wa marehemu umehifadhiwa chumba cha maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Sokoine.

Katika Tukio Lingine imeelezwa kuwa mnamo tarehe 15.04.2016 majira ya saa 11:30 huko Kingurungundwa katika Mto Mbwemkuru uliopo Wilaya ya Lindi vijijini, Mkuu wa Gereza la Kingurungundwa DAIMU ATHMANI MMOROSHA SP, 44YRS, MMAKUWA, MUISLAM wa KINGURUNGUNDWA akiwa na askari magereza waliupata mwili wa Askari magereza No. B 8684 WDR SAMSON STEPHANO KALIBANGU, 24YRS, MJALUO, MKAZI WA KINGURUNGUNDWA akiwa amefariki baada ya kusombwa na maji katika Mto Mbwemkuru tarehe 13.04.2016 majira 14:00hrs wakati akijaribu kumfukuza na kumkamata mfungwa aliyekuwa akitoroka mwenye No. 11/2015 ISSA ABDALLAH HASSANI aliyekuwa amefungwa kwa makosa ya wizi miaka mitano na kutoroka chini ya ulinzi mwaka mmoja. 

Uchunguzi wa daktari umebainisha sababu ya kifo ni kukosa hewa kutokana na kuzama majini. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sokoine. 

About Author

Advertisement

 
Top