Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: UKAWA WAFANYA MAAMUZI HAYA MARA BAADA YA KUONA MAPUNGUFU HAYA BUNGENI
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni amekataa kuwasilisha hotuba ya kambi ya upinzani Bungeni pamo...
Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni amekataa kuwasilisha hotuba ya kambi ya upinzani Bungeni pamoja na upinzani kutoshiriki katika mjadala wa bajeti ya ofisi ya waziri mkuu mpaka serikali itapounda chombo cha kisheria kitakachowezesha uwepo wa serikali ya awamu ya tano na idara zake kwa mujibu wa kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka nje ya ukumbi wa bunge, kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni Mhe, Freeman Mbowe amesema serikali ya awamu ya tano bado inatumia chombo kilichoundwa na serikali ya awamu ya nne, wakati kunamabadiliko mbalimbali yameshafanyika baadhi ya wizara ikiwemo wizara ya tamisemi kuhamishwa kutoka ofisi ya waziri mkuu kwenda ofisi ya rais.

Akizungumzia kuhusu matangazo uamuzi wa bunge kusitisha matangazo yake kurushwa moja kwa moja, Mhe Mbowe amesema kitendo cha bunge kutorushwa moja kwa moja ndani ya ofisi za bunge pamoja na kwa wananchi ni ukiukwaji wa uhuru wa habari na maamuzi hayo hayajapitishwa tume ya huduma za bunge ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kufanya mabadiriko mbalimbali.tc. 

Awali akiwasilisha mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya waziri mkuu kwa mwaka 2016/17, waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema serikali itaendelea kuwawajibisha watumishi wasioendana na falsafa na mwelekeo wa serikali ya wamu ya tano inayotaka kuifikisha Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

Aidha amesema itaanza kutumia mfumo wa kielectroniki wa kufuatilia uwajibikaji na utendaji kazi kwa mujibu wa sera, sheria, kanuni na miongozo kuanzia mwezi julai mwaka huu kwa lengo la kuhakikisha utendaji kazi unaendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano katika kufikia malengo.

MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY

About Author

Advertisement

 
Top