Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: STORI KUBWA KWENYE UCHAMBUZI WA MAGAZETI APRIL 28, 2016 #PowerBreakfast (+Audio)
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
April 28 2016 millardayo.com imekurekodia uchambuzi wa magazeti kutoka Power Breakfast ya Clouds F...
April 28 2016 millardayo.com imekurekodia uchambuzi wa magazeti kutoka Power Breakfast ya Clouds FM, ni uchambuzi wa Habari zote kubwa kupitia magazeti yaliyoandikwa leo Tanzania, Hizi ni baadhi ya Habari kubwa zilizoandikwa leo.
Vee Money
Mbowe apiga bao la kwanza bungeni, Hatua ya Bunge kufikiria namna ya kuwalipa posho wabunge kutokana na uchangiaji wao kwenye mijadala mbalimbali imetafsiriwa kama ni bao la kwanza la kambi ya upinzani Bungeni mwaka huu

Waalimu 40,000 kuajiriwa mei, Jumla ya walimu elfu arobaini wanatarajiwa kuajiriwa na Serikali kuanzia mwezi mei ujao, ikijumlisha wa cheti, stashahada na shahada ili kukabiliana na upungufu wa walimu uliopo katika shule za msingi na sekondari nchini.

Sukari kiasi kidogo kuagizwa nje, Serikali imesema haitatoa kibali cha kuagiza mchele kutoka nje ya nchi lakini itaingiza kiasi kidogo cha sukari ili kufidia nakisi iliyopo nchini hivi sasa kwa lengo la kuepusha mfumuko wa bei ya bidhaa hiyo huku ikieleza kuwa baadhi ya wafanyabiashara wanaficha sukari ili kusubiri bei ipande

Unaweza ukabonyeza Play hapa chini kusikiliza na pia unaweza ukaniachia comment yako hapa..

About Author

Advertisement

 
Top