Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: SIMBA SC BYE BYE KOMBE LA FA, YACHAPWA 2-1
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya soka ya Simba SC imetupwa nje ya michuano ya FA baada ya kupokea kichapo toka kwa timu ya C...
Timu ya soka ya Simba SC imetupwa nje ya michuano ya FA baada ya kupokea kichapo toka kwa timu ya Coastal Union.
Mashabiki wa  Simba SC
Katika mchezo huo wa vuta nikuvute Coastal ilikuwa ya kwanza kutikisa nyavu za Simba baada ya mchezaji Yusuf kupiga mpira wa adhabu ambao ulitinga moja kwa moja nyavuni na kumwacha mlinda mlango wa Simba Sc akiwa ameshika kiuno pasipo kujua lakufanya.

Mpaka timu zinakwenda mapumziko, Coastal Union ilikuwa ikiongoza kwa Goli 1 - 0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo timu ya soka ya Simba ilifanya mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwa coastal ambapo katika dakika ya 49 mshambuliaji Kiiza alifanikiwa kusawazisha goli na kufanya ubao wa matangazo usomeke 1-1.

Mnamo dakika ya 82 Coastal union alifanikiwa kupata Penalt Baada ya mlinzi wa Simba kumchezea ndivyo sivyo Mchezaji wa Coastal Union jambo lililopelekea kupata bao la pili na la ushindi.

Kwa matokeo haya, Simba inatupwa nje ya michuano ya FA na endapo haitachukua ubingwa wa bara haitashiriki kwa mara nyingine katika michuano ya kimataifa.
Mashabiki wa  Simba SC

About Author

Advertisement

 
Top