Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: RAIS ASITISHA SHAMRA SHAMRA ZA SIKU YA MUUNGANO, FEDHA KUPELEKWA KATIKA MRADI WA BARABARA, MAPUMZIKO YAKO PALE PALE
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Rais John Magufuli ameahirisha shamrashamra za kikukuu ya kumbukumbu ya siku ya Muungano wa Tanga...
Rais John Magufuli
Rais John Magufuli ameahirisha shamrashamra za kikukuu ya kumbukumbu ya siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambazo hufanyika kila mwaka, Aprili 26.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, Rais Magufuli amewataka wananchi kusherehekea siku hiyo kwa kupumzika majumbani kwao na katika shughuli zao binafsi.

Aidha, fedha zilizokuwa zimepangwa kwa ajili ya kugharamia vyakula, vinywaji, gwaride na mengineyo ameagiza zielekezwe katika upanuzi wa barabara ya Mwanza ‘Mwanza – Airport’, katika eneo linaloanzia Ghana Quarter hadi katika uwanja wa ndege jijini humo, kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari.

Hii ni Taarifa Rasmi toka Ikulu
Taarifa

About Author

Advertisement

 
Top