Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: MSANII HUYU WA KUNDI LA BLU 3 JACKIE CHANDIRU NAYE YUKO HOI KWA MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Madawa ya kulevya si janga linaloviumizwa vichwa vya wadau wa muziki wa Bongo Flava, bali Uganda pi...
Madawa ya kulevya si janga linaloviumizwa vichwa vya wadau wa muziki wa Bongo Flava, bali Uganda pia mambo si mambo.
Jackie Chandiru
Muimbaji wa zamani wa kundi la Blue 3, Jackie Chandiru yupo kwenye hali mbaya baada ya kuathirika na utumiaji wa unga. Amekuwa kwenye wakati mgumu zaidi baada ya ndoa yake kuvunjika na sasa yupo rehab huku afya yake ikiwasononesha wengi.
Jackie Chandiru
Yupo kwenye kituo cha Bunamwaya ambako madaktari na washauri nasaha wanamsaidia arudi kwenye hali yake ya kawaida. Waliomuona wanadai kuwa hata ngozi yake imeanza kubabuka. Amekuwa akitumia cocaine na madawa mengine.

About Author

Advertisement

 
Top