Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: MKUU WA MKOA WA MWANZA AMSIMAMISHA KAZI AFISA ARDHI NA MWINGINE AAGIZA AKAMATWE KWA TUHUMA ZA RUSHWA
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza kuhakikisha anashi...
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza kuhakikisha anashirikiana na kamanda mwenzake wa Mkoa wa Singida, Mkuu wa TAKUKURU pamoja na Katibu Tawala wa mkoa kwa ajili ya kumkamata na kumrejesha Manispaa ya Ilemela Afisa Ardhi mteule wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Aniceth Rweyemamu ili kujibu tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni 12.
John Mongella
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella

Mongella ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wakuu wa idara, madiwani, maafisa watendaji wa kata na mitaa wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, kufuatia afisa ardhi huyo mteule kudaiwa kupokea kiasi cha shilingi milioni 12 toka kwa mkazi wa jijini mwanza Jesca Tongora ili ampatie kiwanja pamoja na hati.

Wakati Rweyemamu akitakiwa kurejeshwa mwanza ili kujibu tuhuma zinazomkabili, afisa ardhi msaidizi wa manispaa ya Ilemela Debora Tongora amesimamishwa kazi na mkurugenzi wa manispaa hiyo wiki moja iliyopita na tayari amekwisha funguliwa kesi ya kuomba na kupokea rushwa na maofisa wa TAKUKURU mkoani Mwanza.

Mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza pia amefika katika soko la samaki la kimataifa la Kirumba Mwaloni na kuzishauri mamlaka zinazohusika na ajira ya afisa uvuvi wa manispaa hiyo Ivon Maha kumpangia kazi nyingine, kwa kushindwa kusimamia mapato ya soko hilo ambapo badala ya kukusanya shilingi milioni 40 kwa mwezi amekuwa akikusanya shilingi milioni 31.

Mweka hazina wa manispaa ya Ilemela Peter Revelian naye amepewa siku 30 kuhakikisha anasimamia vyema ikiwa ni pamoja na kuyafahamu barabara mapato ya manispaa hiyo baada ya kushindwa kujibu swali la Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella aliyetaka kufahamu mapato ya manispaa hiyo katika kipindi cha mwezi Januari na Februari mwaka huu.

About Author

Advertisement

 
Top