Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: MAISHA NA MAHABA: MUME WANGU ANANINYIMA UNYUMBA...JE NIFANYEJE?
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Habari zenu, Mimi ni mwanamke mwenye watoto wawili na nipo kwenye ndoa kwa miaka nane sasa. Tumek...
mwanamke
Habari zenu,
Mimi ni mwanamke mwenye watoto wawili na nipo kwenye ndoa kwa miaka nane sasa. Tumekuwa tukiishi maisha ya ugomvi kwa muda na mume wangu, ila nikaona ni vyema nijishushe na nisihoji chochote.

Mimi ndiye ninahangaika na familia na mambo yote hakai kujadili jambo lolote la maana na mimi.

Binafsi niliona nijishushe na nisihoji chochote ila tatizo limekua ni kwenye unyumba. Kwa kweli navumilia sana tunalala pamoja najitahidi kujiweka safi, kubadili mazingira ya chumba, manukato na hata mavazi lakini wapi!

Naweza nikamfanyia vikorombwezo vyote ila atageukia upande wa pili na kukoroma nimemsihi sana yeye anasema anawaza maisha hawezi kuendekeza ngono.

Tunaweza kukaa mpaka miezi mitatu hatujakutana, hili swala linanikondesha jamani.

Naombeni njia ya kujinasua katika hili janga.

About Author

Advertisement

 
Top