Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: KOBE BRYANT KUSTAAFU KIKAPU LEO NA HIZI NDIO REKODI ZAKE
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Kobe Bryant atastaafu kikapu siku ya Jumatano usiku dhidi ya Utah Jazz Nyota wa Los Angeles La...
Kobe Bryant
Kobe Bryant atastaafu kikapu siku ya Jumatano usiku dhidi ya Utah Jazz
Nyota wa Los Angeles Lakers Kobe Bryant atastaafu kuichezea Ligi ya NBA leo siku ya Jumatano.

Mechi ya mwisho ya Kobe, 37, itakuwa kati ya Lakers na Utah Jazz katika Uwanja wa Staples Center jijini Los Angeles, California.


Kobe Bryant
Kobe amekuwa bingwa wa NBA mara tano, akisherehekea ubingwa wake 2009

Ni bingwa mara tano na ameichezea All Star mara 18 wakati akiwika katika kikapu.

Bryant amefunga pointi 33,570 katika maisha yake ya uchezaji mpira wa kikapu (miaka 20) katika historia ya NBA, na kumfanya kuwa mcheza kikapu wa tatu katika historia ya NBA.
Kobe Bryant na Michael Jordan
Kobe Bryant alirithi viatu vya Michael Jordan baada ya nyota huyo kustaafu Chicago Bullls

Kobe Bryant ameichezea LA Lakers kwa miaka yote hiyo ambapo alisajiliwa mwaka 1996.

About Author

Advertisement

 
Top