Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: KIIZA NA MURSHID KUKUMBANA NA RUNGU LA ADHABU SIMBA SC
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
RUNGU la adhabu linawasubiri wachezaji wa timu ya soka ya Simba, Hamisi Kiiza na Juuko Murshid am...
RUNGU la adhabu linawasubiri wachezaji wa timu ya soka ya Simba, Hamisi Kiiza na Juuko Murshid ambao hawajaungana na wenzao mazoezini hadi sasa.
Hamisi Kiiza
Wachezaji hao raia wa Uganda walikuwa kwao kuiwakilisha timu yao ya taifa ‘The Cranes’ kwenye mechi ya kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) 2017 dhidi ya Burkina Faso na walitakiwa kurudi baada ya mechi hiyo iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zilisema jana kuwa wachezaji hao wamekaidi agizo la uongozi wao ambapo walitakiwa kuripoti baada ya mechi yao hiyo ya kimataifa mwishoni mwa wiki iliyopita.
“Mpaka sasa hawajajiunga na wenzao na hakuna taarifa zozote za kwa nini hawajarudi nchini,” alisema mtoa taarifa wetu, ambaye aliomba jina lake lisitajwe.

Alisema tayari wachezaji hao wameshaandikiwa barua ya kuwataka kujieleza kwa nini wasichukuliwe hatua kwa kuchelewa kuungana na wenzao katika maandalizi ya mechi za Ligi Kuu na zile za Kombe la FA.
“Barua tumewapelekea wao na tumepeleka kwa Shirikisho la Soka Uganda (Fufa), hivyo tunasubiri maelezo yao na tutachukua hatua, hatuwezi kuvumilia utovu wa nidhamu wa hali hii,” alisema.

Kocha Mkuu wa timu hiyo ambaye pia ni raia wa Uganda, Jackson Mayanja alikaririwa akisema amefanya juhudi za kuwasiliana na kocha wa Uganda, Milutin Sredjovick ‘Micho’ kujua kilichowakwamisha wachezaji hao, lakini alionesha kushangaa Kiiza na Murshid kushindwa kuripoti.

About Author

Advertisement

 
Top