Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: JUVENTUS WATWAA UBINGWA LIGI YA ITALY MARA 5 MFULULIZO BAADA YA NAPOLI KUCHAPWA 1 - 0 NA AS ROMA
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
LEO Juventus wametwaa Ubingwa wa Serie A huko Italy kwa mara ya 5 mfululizo baada ya Timu ya Pili...
LEO Juventus wametwaa Ubingwa wa Serie A huko Italy kwa mara ya 5 mfululizo baada ya Timu ya Pili kwenye Ligi Napoli kufungwa 1-0 na AS Roma huko Stadio Olimpico Jijini Rome.
Juventus
Jana Juve waliifunga Fiorentina Bao 2-1 na kuhitaji Pointi 1 tu ili kujihakikishia Ubingwa lakini kipigo cha Leo cha Napoli kimehakikisha hawawezi tena kuikamata Juve huku Mechi zikibaki 3.

Juve sasa wana Pointi 85 wakifuatiwa na Napoli wenye Pointi 73 na AS Roma wana Pointi 71.

Kwa kutwaa Ubingwa Msimu huu, Juve walionyesha umahiri mkubwa kwani hapo Oktobo 28 walikuwa Nafasi ya 12 wakiwa Pointi 11 nyuma ya Vinara wa Serie A.
Juventus
Lakini baada ya hapo, Juve walishinda Mechi 24 kati ya 25 za Ligi zilizofuatia na kutoka Sare 1.

Katika Mechi ya Leo, Bao la ushindi la AS Roma lilifungwa Dakika ya 89 na Radja Nainggolan kutokana na ushirikiano mwema wa Mkongwe Totti, Pjanic na Mohamed Salah.
Juventus
Shabiki wa Juventus akishangilia Baada ya Timu hiyo kutawazwa mabingwa wa ligi hiyo kwa mara 5 Mfululizo.

VIKOSI: AS Roma: Szczesny; Florenzi, Manolas, RĂ¼diger, Digne; Keita, Pjanic, Nainggolan; El Shaarawy, Perotti, Salah.

Napoli:
Reina; Hysaj, Albiol, Koulibaly, Ghoulam; Allan, Jorginho, Hamsik; Callejon, Higuain, Mertens.

About Author

Advertisement

 
Top