Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: FA CUP:: COASTAL VS YANGA PAMBANO LAVUNJWA, AZAM YAIBUKA KIDEDEA DHIDI YA MWADUI FC
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Mchezo wa nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup (FA Cup) kati ya Coastal Union dhidi ya Ya...
Azam Sports Federation Cup
Mchezo wa nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup (FA Cup) kati ya Coastal Union dhidi ya Yanga umeshindwa kumalizika kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga kutokana vurugu za mashabiki.

Mwamuzi wa pambano hilo alilazimika kulivunja pambano hilo likiwa kwenye dakika 30 za nyongeza baada ya dakika 90 za kawaida kumalizika huku timu hizo zikiwa sare kwa kufungana goli 1-1.

Hadi mchezo huo unavunjwa na mwamuzi, Yanga walikuwa wanaongoza kwa magoli 2-1.

Coastal Union walikuwa wa kwanza kupata goli la kuongoza lililofungwa na Sabo dakika ya 54 kipindi cha pili lakini Ngoma akaisawazishia Yanga kabla ya Tambwe kuiweka mbele Yanga kwa goli la dakika za nyongeza kabla ya mchezo kuvunjwa.

TFF inasubiriwa kutoa muongozo juu ya mchezo huo ambao dakika zake 120 hazikumalizika.

AZAM FC YASHINDA 

AZAM FC imesonga Fainali ya Kombe la Shirikisho, Azam Sports Federation Cup, ASCF, baada ya kuibwaga Mwadui FC kwa Penati 5-3 baada ya Sare ya 2-2 katika Dakika 120 za Mchezo lakini huko Mkwakwani, Tanga, Mechi ya Coastal Union na Yanga ilivunjika baada ya kuchezwa Dakika 15 tu za Dakika za Nyongeza 30 huku Yanga wakiongoza 2-1.

Huko Mwadui Complex, Mwadui, Azam FC walitangulia kuifunga Mwadui FC kwa Bao la Dakika ya 3 la Mcha na Mwadui FC kusawazisha Dakika ya 82 kupitia Kabunda.

Mechi ikaenda Dakika za Nyongeza 30 na kila Timu kufunga Bao 1 zaidi kwa Mcha kuipa Azam Bao la Pili Dakika ya 97 na Mwadui kusawazisha kwa Penati ya Dakika ya 123 kwa Bao la Aziz.

Ndipo zikaja Penati Tano Tano, na Azam kufunga zao zote 5 wakati Kelvin Sabato alikosa 1 kwa Mwadui na hivyo kuipa Azam FC ushindi wa Penati 5-3.

About Author

Advertisement

 
Top