Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: CHADEMA WAANZA KUMKUBALI RAIS MAGUFULI
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
BAADHI ya viongozi na makada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani Tarime mkoan...
Chadema
BAADHI ya viongozi na makada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani Tarime mkoani Mara wameeleza kuridhishwa na utendaji wa Rais John Magufuli kutokana na ushahidi unaoonekana kwa vitendo katika nia yake ya dhati ya kupambana na ufisadi na kasi katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mjini hapa, walisema imefika wakati wananchi na viongozi kuweka tofauti zao za kisiasa pembeni katika masuala muhimu ya maendeleo kwa taifa ikiwemo kulinda rasilimali za taifa na kuongeza uwajibikaji katika serikali ili kuleta ufanisi katika maendeleo ya nchi.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Uwanja Ndege katika Halmashauri ya Mji wa Tarime, Musa Mgunyi (Chadema) alisema kwa sasa jinsi hali ilivyo hakuna sababu ya kutilia shaka uongozi wa serikali iliyopo madarakani, badala yake akawataka wananchi wote bila kujali itikadi za vyama wamuunge mkono Rais Magufuli.

Alisema ingawa alipata ridhaa ya uongozi kupitia Chadema, hakuna sababu kwa sasa kuendekeza siasa za mgawanyo wa kiitikadi bali kumuunga mkono rais kutokana na kutetea yale yote ambayo yalipiganiwa na vyama vya upinzani hapo kipindi cha nyuma ikiwa ni pamoja na kupambana na ufisadi.

About Author

Advertisement

 
Top