Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: BREAKING NEWS:: MKURUGENZI WA HALAMASHAURI YA WILAYA YA LINDI ASIMAMISHWA KAZI
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Kufuatia kero aliyoelezwa mh. Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Kasim Majaliwa na wakazi wa eneo la Nar...
Kufuatia kero aliyoelezwa mh. Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Kasim Majaliwa na wakazi wa eneo la Narunyu Kata ya Kiwalala kuhusiana na Mradi wa Umwagiliaji ambao umetumia kiasi cha Tsh Milioni 566 lakini bila ya kukamilika.
Mkuu wa Mkoa Ndg Gadfrey Zambi

Mkuu wa Mkoa Ndg Gadfrey Zambi

Siku ya jana Mkuu wa Mkoa Ndg Gadfrey Zambi ametimiza ahadi yake aliyomuahidi Mh Waziri Mkuu kuwa ataufuatilia na kuchukua maamuzi juu ya waliochelewesha au kudhorotesha mradi huo kushindwa kukamilika kwa wakati ilihali umetumia kiasi kikubwa cha pesa.

Akitoa maamuzi leo hii Mkuu wa Mkoa amesema kuwa watu wa Umwagiliaji wemaisababishia Hasara kubwa Serikali na pia Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi Oliva Vavunge alishindwa kuwajibika ipasavyo hivyo amemsimamisha kazi kuanzia leo (jana) hadi hapo uchunguzi utakapomalizika.

Bi Oliva Vavunge
Bi Oliva Vavunge akisalimiana na Mh. Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa.

Mradi huo ulianza kujengwa mwezi wa 6 mwaka 2011 hadi kufikia leo hii haujakamilika licha ya kutumika zaidi ya Tsh milioni 561.


UNAWEZA MSIKILIZA HAPA MKUU WA MKOA

About Author

Advertisement

 
Top