Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: BIDHAA FEKI ZAKAMATWA WILAYANI KILWA, ZINGIIKIZWA KWA NJIA ZA PANYA
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi limefanya operesheni ya kukagua uingizwaji wa bidhaa haramu, Opere...
Bi Renata Mzinga
Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi limefanya operesheni ya kukagua uingizwaji wa bidhaa haramu, Operesheni hiyo imefanyika Wilayani kilwa na kufanikiwa kukamata bidhaa Haramu mbalimbali ambazo zinaleta madhara kwa watumiaji na kuikosesha serikali mapato (Kodi) kwa kuwa bidhaa hizo zimeingia kwa njia za panya.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Mkoani Lindi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Bi Renata Mzinga amesema wamefanikiwa kukamata bidhaa mbalimbali ikiwemo mafuta ya kupikia na sukari.

Aidha Kamanda Mzinga amewaomba wananchi wa Lindi na Viongozi wake kushirikiana na Polisi kwa kutoa Taarifa mbalimbali ambazo zitafanikisha kudhibiti hali hiyo na Nyinginezo ambazo zinafanywa kinyume na Taratibu za Serikali.

MSIKILIZE HAPA AKITOA TAARIFA HIYO KAMANDA MZINGA.

About Author

Advertisement

 
Top