Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: BABUTALE AZUNGUMZIA HAKEEM UWEZEKANO WA KUMUALIKA KATIKA SHOW KUBWA YA DIAMOND PLATNUMZ "DIAMOND FOREVER"
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Diamond Platnumz na meneja wake, Babutale huhakikisha wanatumia kila fursa inayojitokeza mbele yao...
Diamond Platnumz na meneja wake, Babutale huhakikisha wanatumia kila fursa inayojitokeza mbele yao. Hivi karibuni wawili hao walikutana na muigizaji maarufu wa tamthilia ya Empire, Yazz anayejulikana zaidi kama Hakeem jijini Los Angeles, Marekani.
Kupitia kipindi cha The Playlist cha Times FM, Babutale ameeleza jinsi walivyokutana na staa huyo na kilichofuata baada ya hapo
Jamaa (Yazz) alikuja kwenye hoteli ambayo sisi tumefikia alikuwa na mambo yake. Mimi sijuagi zile movie nisiwe muongo, nimemuona tu hivi akina Diamond wanaongea naye. Mchana nimeona mabango yake mji mzima, LA nzima amechafua Billboard, kwahiyo nikamkumbua huyu nimemuona mchana, hizi series zenu sijui za nini sijawahi kuziona nisiwe muongo, bado ya kumuona kule niliporudi home ndio ikabidi niangalie Empire vizuri. Pale tulipokuwa tunaongea tukachange namba, tukamwambia sisi tunatokea Afrika nini akasema ‘I wish to be in Africa’ nikamwelezea huyu ni msanii wangu mkubwa, baada ya kuangalia profile ya Diamond akawaka vile. Haijaishia hapo, tukabadilishana na namba na mchizi anatamani kuja hata Bongo yaani anytime. Tunachat naye kidogo, soon tunaenda Marekani kuna kitu tunaenda kufanya najua tutakutana naye tutamaliza maongezi yetu., hauwezi jua labda Diamonds are Forever inayokuja mwaka huu tunaweza tukamwalika.

About Author

Advertisement

 
Top