Loading...

JE WEWE NI SHABIKI WA DRAKE NA BEYONCE? HII HAPA JOINT YAO MPYA ISIKILIZE HAPA

Wimbo mpya wa Drake aliofanya na Beyonce umevuja mtandaoni saa chache zilizopita, wimbo unaitwa “Can I”, wimbo pia unasauti ya msanii Sal Houdini. Kwenye wimbo huu Beyonce anasema maneno haya tu “Can I. Baby”. Wimbo umetajwa kuwepo kwenye album mpya ya Drake ‘Views From the 6′.

LICHA YA MFULULUZI WA AJALI MBAYA MWEZI MARCH/APRIL. TAKWIMU ZAONESHA KUPUNGUA KWA AJALI ZA BARABARANI MWAKA 2015

Licha ya mfululizo wa ajali mbaya zilizotokea kati ya mwezi March na April Mwaka huu lakini Takwimu zinaonyesha kupungua kwa kiwango kikubwa kwa ajali za barabara kwa mwaka 2015 ukilinganisha na Mwaka 2014 katika kipindi kama hicho.
Ajali
Akisoma bajeti wa Wizara ya Mambo ya Ndani leo Bungeni Waziri wa Mambo ya ndani Mh. Mathius Chikawe amesema Takwimu zinaonyesha kuwa 2718 ya ajali zote ukilinganisha na ajali 6050 zilizotokea katika kipindi kama hicho kwa mwaka jana.

Mh. Chikawe amesema ili kudhibiti na kupunguza zaidi ajali za barabarani serikali imechukua hatua kadhaa ili kukomesha matukio hayo ambayo kwa mwaka huu pekee watu 2883 walipoteza maisha wakati watu 9370 wamejeruhiwa.

MWANASIASA MKONGWE AZUNGUMZIA MAKUNDI YA URAIS NDANI YA CCM

Kingunge Ngombare
Pichani ni mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombare
Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombare Mwiru ametamka ya kwamba Chama Cha Mapinduzi(CCM) kamwe hakiwezi kuepuka makundi ya urais kupitia chama hicho wakati kikielekea katika hatua za ukingoni za kulipata jina la mgombea atakayepeperusha bendera ya urais katika uchaguzi wa mwaka huu kwa kuwa hata miaka ya nyuma yalikuwepo.

Kauli ya mwanasiasa huyo inakuja wakati kamati kuu ya chama hicho ikikutana mjini Dodoma kuandaa ajenda za mkutano wa halmashauri kuu ya CCM huku ajenda ya jina la nani atakayekipa ushindi mwaka huu katika nafasi ya urais ikitajwa kutawala katika mkutano huo.

Mwanasiasa huyo alitoa kauli hiyo juzi wakati akihojiwa katika kipindi cha uzalendo kinachorushwa na luninga ya ITV wakati akizungumzia makundi ya urais ndani ya CCM kuelekea uchaguzi mkuu.

Akihojiwa katika kipindi hicho alisema kuwa CCM hakiwezi kwenda kwenye uchaguzi mkuu bila ya kuwa na makundi kwa kuwa makundi hayo yalianza tangu mwaka 1995 hadi sasa.

“Hatuwezi kwenda kwenye uchaguzi wa kidemokrasia bila ya kuwa na makundi,mwaka 1995 kila mgombea alikuwa na kundi lake na mwaka 2005 tulikuwa na makundi hata mwaka huu unayo makundi”alisema Mwiru

Alisema kuwa katika mfumo wa kidemokrasia ndani ya chama unaruhusu makundi kwa kuwa kila mgombea anakuwa na kundi lake ambalo linamjenga na kutoa ushawishi katika harakati mbalimbali.

Alisema kuwa kuna tofauti kubwa kati ya makundi ya urais ya mwaka 1995 na ya mwaka 2015 kwani miaka hiyo makundi yalikuwa ni ya kawaida tu tofauti na sasa ambapo baadhi ya wanachama wamekuwa na mitizamo hasi .

Mwanasiasa huyo alisisitiza kuwa mbali na makundi hayo mwisho wa siku ni lazima apatikane mgombea mmoja ambaye atakubalika nje ya CCM.

“Mwisho wake ni lazima apatikane mmoja kupitia vikao vya CCM na anayekubalika na wengi ndani ya CCM ndiye atakayekubalika nje ya CCM hiyo ndiyo demokrasia”alisisitiza Mwiru
>>(Habari na jamiiblog)

WALEMAVU WAFUNGA BARABARA JIJINI DAR, WAKIILALAMIKIA SERIKALI KWA KUVUNJA VIBANDA VYAO

WalemavuUmati wa Walemavu wamefunga makutano ya barabara katika mataa ya Ilala na kusababisha magari kutokupita...Walemavu hao wanadai vibanda vyao vya kufanyia biashara vimevunjwa na jiji usiku na kuchukua baadhi ya bidhaa zao ... Madai yao makuu ni kwa serikali kwamba haiwajali, Bora iwaue tu kuliko kuachwa wakiishi kwa tabu huku vibanda vyao vilivyopo sokoni Karume vikibomolewa.
>>Clouds TV

KITALE ATOA VITISHO KWA MTU HUYU BAADA YA KUSAMBAZA PICHA TATA ZA STAN BAKORA ZINAZOMUONESHA ANABANJUKA NA KIBINTI GARINI

Picha za Msanii wa vichekesho anaeibukia, Stan Bakora akiwa anabanjuka na mwanamke ndani ya gari zimesambaa kwa kasi mtandaoni na kupelekea msanii mwenzake, Kitale “Mkude Simba” ambaye ndiye aliemtoa kisanii kuingilia kati na kumshukia Mateja Musa ambaye anadaiwa kuziweka picha hizo mtandaoni.
Stan Bakora
“@matejamusa wewe ni Ndugu yangu lakini leo umenikosea kwa ulichokiandika kwenye acount yko ya insta kuhusu @stanbakora umenikosea plz! naomba ufute zile picha haraka nakupigia cm yng upokei sio poa haya maisha laiti ungekuwa unaona cm anazopigiwa dogo na watu tofautitofauti ungemuonea hata huruma huyu bado dogo ajakomaa na hivyo vitu mnamchanganya mpaka tunashindwa kufanya kazi zingine tokea asubuhi dogo anaumwa presha kwa mipicha yako hiyo unayoipost na aliyekupa hizo picha namjua mwambie ajifiche atakavyojificha leo au kesho namtia mikononi waulize wenzio wanakijua hiki kichwa dakika moja mbele....mpaka saa 4 ujafuta hizo picha @matejamusa basi we jiandae na ugeni kutoka mwananyamala”.

MAPENZI au PESA? GAVANA WA NIGERIA ALIYEMUOA MREMBO ALIYEMZIDI UMRI MIAKA 27 ASEMA YAMOYONI (Pichaz)

Gavana wa jimbo la Edo la nchini Nigeria, Adams Oshiomhole, amemuelezea mke wake, Iara, kama mlimbwendwe kwenye moyo wake na kwamba si kwamba hajamuoa kuziba pengo la mke wake aliyefariki.
Adams Oshiomhole
Akiongea kwenye misa ya shukrani kwenye kanisa la Immaculate Conception Cathedral, Auchi, Jumapili iliyopita, Oshiomhole alizipuuzia ripoti kuwa mke wake ni model maarufu na kudai kuwa maneno hayo yametokana na urembo wa mke wake. 
Adams Oshiomhole
“Ninaposoma habari za kwenye magazeti na wanasema kuwa Comrade ameoa ‘mlimbwende’ mimi nasema labda ni mtu mwingine,” alisema. 

“Msichana ambaye Mungu amleta kwangu kumuoa hakuwahi na si mlimbwende. Of course, ni mrembo na naelewa kwanini watu wanadhani msichana wa aina hii anaweza kuwa model, of course, ni model moyoni mwangu na tuna tumaini na kuomba kwenye moyo wa Mungu wetu na nadhani hicho ndio kitu muhimu.”
Adams Oshiomhole
Gavana huyo ana umri wa miaka 63 huku mke wake huyo mpya ana miaka 36. Mrembo huyo ni raia wa Cape Verde na alifunga naye ndoa weekend iliyopita.

Ndoa yao ilifungwa mbele ya wageni akiwemo rais wa Nigeria Muhammadu Buhari na mtu tajiri zaidi Afrika, Aliko Dangote.

Ndoa hiyo imekuwa gumzo kwenye bara zima la Afrika.
>>bongo5

ADAM JUMA ATOA KAULI NZITO KUPITIA INSTAGRAM JE UNATAKA KUJUA INAMHUSU NANI BOFYA HAPA

Muongozaji wa video bora na mkongwe Tanzania ametoa ujumbe wa kuonyesha amekerwa na jambo flani kwenye tasnia ya sanaa haswa kwenye upande wa utengenezwaji wa video Tanzania. Adam Juma alitumia Instagram yake kuandika haya Maneno makali
adam juma
"Watanzania wabishi sana, miaka mitatu tu mtu anaanza kujifanya anajua kumpita mungu,,, kwa style hii hakuna atakae toka i swear to god!!!! Mimi kila siku najifunza ili siku moja nifanye kazi ninayoipenda kwa umakini sio kutengeneza video tu!!!!"
Adam anaendelea kufunguka kuwa “Wengine wanaona kushika kamera na kushot ndio mwisho, tunafanya kazi na watu wengine njee tunajifunza sana vitu mkiona nimenyamaza mnaona km fala vile, ngoja sasa, ota vuzi kwanza pata watoto waende shule, jenga nyumba, acha kunya choo cha baba, kama ni shabiki unadomo peleka kwenye sehemu flani amazing za unaempenda kabla kuhujanitest!!! Muda wa majeruhi ukiingia kwenye 18 zangu nakupendezesha alafu tunakuaga leaders..”

Je kwa kauli hizi Unahisi kuna director au msanii kamkera Adam Juma?,
Picha kwahisani ya BONGO5, Post: Sammisago.com

TFDA YATEKETEZA VIDOZI,VYAKULA NA MADAWA YASIYOFAA KWA MATUMIZI YA BINADAMU.

Na.Ahmad Mmow,Lindi.
Mamlaka ya chakula na madawa nchini (TFDA) jana ilichoma moto vyakula, vinywaji na vipodozi visivyositahili kwa matumizi ya kibinadamu.
taswira ya Lindi
Taswira Maridhawa Kutoka Katikati ya Mji wa Lindi

Zoezi hilo ambalo utekelezaji wake ulisimamiwa na maafisa wa afya wamkoa wa Lindi, halmashauri ya manispaa ya Lindi na mamlaka ya chakula na dawa kanda ya kusini lilifanyika katika manispaa ya Lindi. Ambapo vipodozi, vinywaji na vyakula vyenye thamani ya shilingi 19.26 milioni, ambavyo muda wake wa matumizi ulikuwa umekwisha, viliteketezwa kwa kuchomwa moto.

Akizungumza na waandishi wa habari walikwenda kushuhudia tukio la uteketezaji huo, kaimu meneja wa mamlaka ya chakula na madawa wa kanda ya kusini, Juma Bukuku. Alisema uteketezaji huo umetokana na msako uliofanyika katika halmashauri ya manispaa na wilaya ya Lindi uliofanyika kuanzia tarehe 13 hadi 15 mwezi huu kwenye maduka mbalimbali yaliyo kwenye halmashauri hizo.

Alisema baadhi ya bidhaa zilichomwa moto zilikwisha muda wake wa matumizi, zisizo sajiliwa na zilizokatazwa kutumiwa hapa nchini kutokana na kuwa na madhara kwa watumiaji.
"kunavipodozi ambavyo vilikatazwa kutumika tumevikuta madukani, baadhi ya bidhaa hazina usajili na hata lugha iliyoandikwa haileweki na bidhaa nyingine zimekwisha muda wake wa matumizi, lakini tumevikuta madukani vinauzwa, jambo ambalo halikubaliki". 

Kaimu meneja huyo alibaisha kuwa wafanyabiashara wengi hawatunzi kumbukumbu muhimu zinazoonesha walinunua wapi. Hivyo kusababisha ugumu wa kujua ni nani wanaingiza bidhaa zilizopigwa marufuku kutumika. Alisema misako itakuwa endelevu, nakuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa mamlaka hiyo na maafisa wa idara ya afya waliokaribu katika maeneo wanayoishi. 

Pia meneja huyo aliwaasa wananchi kusoma maelezo yaliyo kwenye vifungashio vya bidhaa wanazonunua ili waweze kujua kama bidhaa hizo zinaviwango vyenye ubora unaokubalika kisheria. Ikiwamo kujua muda wa matumizi, mahali zilikotengenezwa, na kama zimesajiliwa.

Bidhaa zilizoteketezwa ni pamoja na vipodozi vyenye thamani ya shilingi 16,181,540.00, Madawa yenye thamani ya shilingi 939,500.00 na vyakula vyenye thamani ya shilingi 2,143,400.00.
Older Posts
© Copyright FAHARI YA KUSINI | Designed By LindiYetu
Back To Top